HabariPilipili FmPilipili FM News

Maafisa Washirika La Bima Ya Afya NHIF Wahimizwa Kuharakisha Kuwasajili Wakenya.

Waziri wa afya Sicily Kariuki sasa anawataka maafisa wa shirika la bima ya afya NHIF kuharakisha mchakato wa kusajili wananchi katika kaunti mbalimbali nchini, kabla ya serikali kuzindua rasmi mpango wa afya kwa wote mwezi ujao wa disemba.

Akizungumza mjini kisumu waziri Kariuki anasema rais Uhuru Kenyatta atazindua mpango huo rasmi, baada ya maadhimisho ya sherehe za jamuhuri, akisisitiza ni laima kila mtu ajumuishwe katika mpango huo.

Kauli yake  imetiliwa mkazo na msemaji wa ikulu Kanze Dena, wakati akiongea na waandhishi wa habari katika ikulu ya rais hapa mombasa.

 

Show More

Related Articles