HabariPilipili FmPilipili FM News

Obado Kujua Leo Kama Ataachiliwa Kwa Dhamana Au La.

Gavana wa migori Okoth Obado atajua hatma yake leo endapo ataachiliwa kwa dhamana au la.

Gavana Obado amelazimika kukesha rumande usiku wa kuamkia leo akisubiri kubaini iwapo ataendelea kuzuiliwa kwa siku 15 zaidi, ili kuruhusu uchunguzi kufanywa dhidi ya madai ya  kupatikana kwa bunduki 8 nyumbani kwake.

Upande wa mashataka ukiongozwa na Catherine Mwaniki unasema polisi wanahitaji muda zaidi ili kufanya uchunguzi wa kutosha.

Mawakili wa Obado ,Cliff Ombeta na Rodger Sagana aidha wamekashifu mahakama kwa kupinga ombi lao la kumwachilia mteja wao kwa dhamana na kudai kwamba amenyimwa haki yake kisheria.

Obado ambaye aliachiliwa kwa dhamnai kwa kesi dhidi ya mauaji ya mwanafunzi Sharon Otieono alikamatwa na kufikishwa mahakamani hapo jana.

Show More

Related Articles