HabariPilipili FmPilipili FM News

Magari Ya Uchukuzi Bado Hayajarejea Barabarani Mombasa.

Magari mengi ya uchukuzi wa umma bado hayajarejea barabarani kaunti ya Mombasa hali ambayo  imeathiri pakubwa shughuli za usafiri.

Wananchi wengi wanalazimika kutembea mwendo mrefu kwa kukosa njia mbadala za usafiri.

Wengi wamelalamikia hatua ya wahudumu wa tuk tuk na boda boda kuongeza nauli maradufu zaidi ya bei za kawaida.

Msako dhi ya  magari na watumizi wa barabara wasiofuata sheria za trafiki unaingia siku ya tano leo kote nchini, hapa mombasa kukishuhudiwa msongamano wa magari katika barabara ya Nyali kuelekea katikati ya mji, kufuatia kizuizi cha polisi wanaokagua magari katika daraja la nyali.

Kufikia sasa ni matatu chache zinahudumu katika maeneo kadha hapa Mombasa kama vile Tudor- Likoni, Bamburi – kuingia mjini pamoja  na route za  Nyali kwenda mjini.

Show More

Related Articles