HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwambire Apata Afueni Mahakamani.

Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire amepata afueni kubwa baada ya mahakama ya Malindi kutupilia mbali kesi yakupinga ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Akitoa uamuzi huo jaji Erick Ogola amesema mlalamishi wa kesi hiyo mbarak issa kombe ambaye ni mpiga kura hakua na ushahidi mzito wakupinda ushindi wa mbunge huyo.

Kwa upande wake mbunge Mwambire hakuweza kuficha furaha yake akisema ni safari ndefu aliyokua akipigana nayo na sasa amewaahidi wakaazi wa Ganze maendeleo zaidi huku akiongezea wapinzani wake pia wanafaa kumuunga mkono kufanyia maendeleo wakaazi wa Ganze.

Mbunge huyo alikua ameandamana na seneta wa Mombasa Mohamed Faki na mwenzake wa Kwale Issa Juma Boi.

Mlalamishi wa kesi hiyo ameagizwa kulipia garama zote za kesi hiyo ambayo ni shilingi milioni 2.5.

 

Show More

Related Articles