HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kuzuru eneo la Pwani Juma lijalo

Rais Uhuru Kenyatta atazuru ukanda wa Pwani juma lijalo ambako ameratibiwa kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo. Kulingana na msemaji wa ikulu Kanze Dena rais Kenyatta atazindua rasmi kikosi cha huduma ya ulinzi wa baharini kitakachoongozwa na naibu mkurugenzi mkuu Brigadier Loonena naisho Jumatatu wiki ijayo. Kikosi hicho kitawakabili wanaotishia usalama na kusababisha uchafuzi wa bahari miongoni mwa majumumu mengine.

Kando na hayo rais Kenyatta pia atazindua maandalizi ya kongamano la uchumi wa baharini.

Akiwa Mombasa rais pia anatarajiwa kuangazia maandalizi yauzinduzi wa mpango wa huduma za afya kwa wote  ambao atazindua rasmi katika kaunti ya Kisumu mwezi ujao.

Show More

Related Articles