HabariMilele FmSwahili

Gavana Obado kusalia korokoroni hadi kesho atakapobaini hatma yake

Gavana wa Migori Okoth Obado atasalia mikononi mwa maafisa wa polisi hadi kesho saa 11 asubuhi atakapobaini hatma yake. Hakimu wa mahakama ya Kibera Joyce Gandani anasema Obado anayekabiliwa na kesi ya kumiliki bastola kinyume na sheria atalala katika kituo cha polisi cha Gigiri. Ni baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Catherine Mwaniki kuiomba mahakama siku 15 kukamilisha uchunguzi dhidi yake. Mwaniki anasema wananuia kubaini iwapo  bunduki nane zinazodaiwa kupatikana katika makaazi ya Obado hapa nairobi na migori zilitumika kutekeleza uhalifu.

Hata hivyo mawakili wa Obado wakiongozwa na Cliff Ombeta wamewatuhumu polisi kwa kuwasilisha ushahidi usiokuwa na msingi na kwamba mteja wao yuko tayari kusaidia katika uchunguzi.

Wakati huo huo baadhi ya wafuasi wa Obado waliokuwa mahakamani wameshutumu vikali kufikishwa kwake mahakamani wakiitaja hatua hiyo kama njama  ya kumhujumu.

Show More

Related Articles