HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Kuzuru Pwani.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru eneo la pwani wiki ijayo haya ni kulingana na msemaji wa ikulu Kanze Dena akiongea na waandishi wa habari katika ikulu ya rais jijini Mombasa.

Dena amedokeza rais Kenyatta anatarajiwa kuzindua rasmi kikosi cha walinzi wa baharini, huku pia akitilia mkazo maandalizi ya kongamano kubwa la kimataifa almaarufu blue economy conference ambalo litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Nairobi na kuhudhuriwa na zaidi ya wajumbe 700 kutoka mataifa mbalimbali ya kigeni.

Dena anasema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili zaidi  faida na matumizi ya raslimali za bahari, mito pamoja na vyanzo vingine vya maji kwa faida za wananchi.

Kando na hayo Dena amekinzana na wanaodai kucheleweshwa kwa baadhi ya miradi ya serikali ikiwemo ujenzi wa barabara, sawia na bandari za shimoni na lamu akisema serikali imesimama kidete kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.

 

Show More

Related Articles