HabariPilipili FmPilipili FM News

CIPK Yapinga Kutoruhusiwa Kuvalia Kwa Kofia Wanaume Wa Kiislamu Wanapoenda Kuchukua Vyeti Vya Usafiri.

Baraza la maimamu na waumini nchini CIPK limepinga hatua ya wanaume wa jamii ya kiislamu kutoruhusiwa kuvaa kofia pale wanapoenda kuchukua cheti cha kusafiria (passport).

Akipinga hatua hiyo katibu mkuu wa baraza hilo Sheikh Mohammed Khalifa amesema kutowaruhusu waislamu kuvalia kofia ni njia mojawapo ya kuwadhalilisha waislamu.

Khalifa ameitaka serikali kuwapatia waislamu uhuru wa kuvaa kofia wanapochukua cheti hicho kama yanavyoruhusiwa madhehebu mengine ya humu nchini.

Show More

Related Articles