HabariPilipili FmPilipili FM News

Madzayo Alisuta Bunge La Kaunti Ya Kilifi.

Seneta wa kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo amewataka wawakilishi wa wadi katika bunge la kaunti hiyo kutumia fursa waliyopewa na wananchi kusuluhisha matatizo yanayowakumba wapiga kura.

Akizungumza alipolihutibia bunge hilo kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake kwa muhula wa pili, Madzayo amesema wawakilishi hao wanajukumu kubwa la kushughulikia matatizo ya ardhi, afya pamoja na elimu katika kaunti hiyo ili kuhakikisha maisha ya mkazi wa kilifi yanaimarika.

Hata hivyo Madzayo amewasuta vikali wawakilishi wadi hao kwa kumuidhinisha Alio Ibrahim, kama afisa mkuu wa sekta ya afya ya umma licha ya kususia kumuidhinisha hapo awali.

Show More

Related Articles