HabariPilipili FmPilipili FM News

Bunge La Kwale Lapitisha Mswada Wakusimamisha Ujenzi Wa Bandari Ya Shimoni.

Bunge la kaunti ya Kwale limepitisha mswada wa kutaka kusimamisha  mradi wa ujenzi wa bandari ya Shimoni  huko Lungalunga,  kwa madai  kwamba  mradi huo ni kati ya miradi ambayo haileti faida kwa  serikali ya kaunti na wakaazi  kutokana na kukosekana kwa  makubaliano ya ugavi wa mapato kati ya serikali kuu na ile ya kaunti.

Mradi wa  bwawa la Mwache  na ule wa kampuni  ya uchimbaji madini ya basetitanium  ni kati ya miradi inayotajwa kukosa  kuwafaidi wenyeji wa kaunti hiyo.

kiongozi wa wengi  katika bunge la kaunti ya kwale Raia Mkungu amesema  serikali ya kitaifa  haifuati sheria wakati wa ugavi  wa mapato  .

Show More

Related Articles