Swahili Videos

Mke adaiwa kumkata bwana kwa jembe na kumuua, Kakamega

Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Muhungula eneo bunge la Malava baada ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 45 kudaiwa kumkatakata kwa jembe na kumuua mumewe kufuatia mzozo wa nyumbani na kisha kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Malava…..
Familia ya mwendazake inadai kuwa marehemu na mshukiwa mkewe Susy Shikuku wameishi wakizozana kila mara katika ndoa yao .
Haya yalijiri huku kijana aliyemaliza darasa la nane hivi majuzi katika kata ya Kimangeti, akizuiliwa na polisi baada ya kumpiga babake mzazi kwa kifaa butu na kumuua kwa kuuza mahindi mikebe miwili .

Show More

Related Articles