HabariMilele FmSwahili

Maafisa 2 wa cheo cha Constable wahukumiwa kifo kwa kosa la mauaji

Maafisa wawili wa cheo cha Constable wamehukumiwa kifo na mahakama hapa Nairobi baada ya kupatikana na kosa la mauaji. Benjamin Kahindi Changawa na Stanley Okoti wote wanaohudumu kituo cha Kabete, Nairobi walimuua polisi mwenzake Constable Joseph Obongo, pamoja na jamaa zake wawili Georfrey Mogio na Amos Okenye mtaani Kangemi kwa tuhuma za wezi mnamo Oktoba mwaka 2014. Hukumu hii imetolea na Jaji S.N Mutuku. Mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi iliyokuwa ikifuatilia kesi hiyo imeelezea kuridhishwa.

Show More

Related Articles

Check Also

Close