HabariMilele FmSwahili

Ruto :Serikali haitaruhusu fedha zilizotengewa miradi ya ajenda nne kuu kufujwa

Serikali kamwe haitoruhusu fedha zilizotengewa miradi ya agenda nne kufujwa na maafisa wake. Naibu rais William Ruto anasema yeye na rais wataongoza vita vikali dhidi ya ufisadi kwa lengo la kufanikisha maendeleo. Akihutubu kwenye mkutano uliowaleta pamoja wajumbe wa mataifa tofauti hapa Nairobi, Ruto amesema kufanikishwa ajenda hizo nne ndio njia ya kipekee ya kuimarisha maisha ya wakenya.

Kadhalika Ruto amesifia juhudi zinazowekwa na idara za DCI,DPP na EACC kuwakabili waliopora mali ya umma akionya dhidi ya vita hivyo kuingizwa siasa.

Usemi wake umeridhiwa na naibu mwenyekiti wa baraza la magavana Ann Waiguru anayetaka magavana washirikishwe kikamilifu ili kufanikisha ajenda hizo za kuboreshwa sekta ya afya,ujenzi wa nyumba za bei nafuu,viwanda na usalama wa chakula.

Show More

Related Articles