HabariPilipili FmPilipili FM News

Fateni Sheria Ama Msitoe Magari Yenu Barabarani, Asema Ipara.

Kwa mara nyingine wenye magari kaunti ya Mombasa wametakiwa kufuata sheria za trafiki na kuhakikisha magari yao yameafikia vigezo vyote hitajika.

Johnstone Ipara ambaye ni kamanda wa polisi hapa mombasa anasema msako dhidi ya magari yasiofuata sheria utaendelea hadi pale nidhamu itadumishwa barabarani.

Ipara ameonya madereva wenye nia ya kurudisha magari yao barabarani bila kutimiza vigezo hitajika, akisema huenda wakalazimika kuyazuilia magari hayo, na hata kufutilia mbali leseni za madereva husika.

Show More

Related Articles