HabariPilipili FmPilipili FM News

80 Wafikishwa Mahakamani Mombasa Kwa Kukiuka Sheria Za Michuki.

Zaidi ya watu 80 walifikishwa katika Mahakama ya Mombasa hapo jana na kufunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria za trafiki.

Wengi kati ya hao ni madereva na wenye magari ambayo yana kasoro ikiwemo kukosa mikanda ya kiusalama yaani safety belt, taa za magari, leseni za kuendesha gari pamoja na bima miongoni mwa vitu vingine.

Mbele ya Hakimu mwandimizi katika mahakama ya Mombasa Christine Ogweno Wengi walitozwa faini ya kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 15,000 kulingana na uzito wa makosa yao.

Yakijiri hayo wengie walokamatwa katika msako wa jana watafikishwa kotini leo, huku msako huo unaolenga magari ya uchukuzi wa umma ukiendelea kote nchini.

Show More

Related Articles