HabariPilipili FmPilipili FM News

Bandari Ya Mombasa Imeboresha Shughuli Za Upakuzi Wa Meli Kubwa.

Badari ya Mombasa imeingia kwenye ubora wa ulimwengu kwenye shughuli za upakuzi hii ni baada ya kuwekeza mabilioni ya fedha kwenye ununuzi wa vifaa vya kisasa vya upakuzi bandarini.

Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu katika idara ya upakuzi wa makasha katika bandari ya Mombasa Edward Opiyo anasema  sasa bandari ya Mombasa inauwezo wa kupakua meli kubwa za kimataifa kwa muda wa masaa 48 pekee kinyume na hapo awali ambapo iligharibu bandari siku zaidi ya kumi na nne kupakua meli moja.

Opiyo anasema  hali imerudi shwari katika kituo cha kuhifadhi makasha cha Nairobi kutokana na sheria khali kuwekewa  wenye makasha ambao walikuwa wakijikokota kuchukua mizigo yao kwenye hifadhi hiyo.

Show More

Related Articles