HabariMilele FmSwahili

Mugo Wa Wairimu kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi

Jamaa anayedaiwa kuwalaghai wakenya kwa kujifanya kuwa daktari James Mugo almaarufu Mugo Wa Wairimu anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapa jijini Nairobi leo. Mugo amekesha katika kituo cha polisi cha Pangani baada ya kukamatwa jana katika mtaa wa Gachie kaunti ya Kiambu. Kati ya mengi Mugo anatuhumiwa kuwanyanyansa kimapenzi wagonjwa na kutoa huduma za afya bila leseni katika hospitali yake.

Show More

Related Articles