
Msako wa magari ya uchukuzi unaoendeshwa unalenga kuzuia ajali nyingi zinazoshuhudiwa barabarani. Akiongea alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uchukuzi waziri wa uchukuzi James Macharia anasema mgomo wa hapo jana ulitokana na magari mengi kukosa kuzingatia sheria za Michuki. Akimbuji mwenyekiti wa kamati hiyo David Pkosing aliyetaka kujua hakikisho lake kwa wakenya Macharia anasema aslimia 95 ya wakenya wanaunga mkono oparesheni hiyo. Anasisitiza kuwa hawatasitisha.