HabariMilele FmSwahili

Watu 14 waorodheshwa kuteuliwa katika nafasi ya katibu wa EACC

Watu 14   wameorodheshwa kuteuliwa kuwa katibu wa tume ya kukabili ufisadi EACC. 14 hao wamechaguliwa kutoka kwa  watu 71 waliotuma maombi ya kuchukua nafasi hiyo. Hii ni kufuatia kuelekea kukamilika kwa  hatamu ya kuhudumu ya katibu wa tume hiyo Halakhe Waqo atakayeondoka afisini mwezi Januari. Miongoni mwa walioorodheshwa ni  naibu afisa mkuu mtendaji Michael Mubea na aliyekuwa kamishna katika tume ya  huduma za polisi murshid Abdalla. Wengine ni pamoja na Okuku Nakitari, Lucy Wanja Kinuthia na Joel Lusweti Mabonga.

Show More

Related Articles