HabariMilele FmSwahili

Utafiti : Wanaume wengi Nairobi hawajui hali yao ya HIV

Idadi ya wanaume wanaojitokeza kupimwa iwapo wana virusi vya HIV kaunti ya Nairobi ni ya chini mno ikilinganishwa na wanawake. Hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na wizara ya afya kaunti ya Nairobi ambao unaonyesha wanaume wengi hawapendi kufahamu hali yao ya kiafya. Afisa wa idara ya afya Lillian Mutua anasema hali hiyo hutokana na wanaume kuogopa kubaguliwa iwapo watapatikana na virusi vya HIV. Ni kutokana na hatua hii idara ya afya ya kaunti imepanga kampeini ya kuwahamasisha wenyeji wa Nairobi kuhusu umuhimu wa kupimwa na pia kutumia dawa za kupunguza makali ARVS kuanzia tarehe 25 mwezi huu.

Show More

Related Articles