HabariMilele FmSwahili

Makachero wa EACC wavamia makaazi ya gavana Obado Migori na Nairobi

Makachero wa tume ya ufisadi wamevamia  leo makaazi ya gavana wa Migori Okoth Obado huko Migori na hapa Nairobi. Makachero hao wanaaminika kusaka stakabadhi zitakazoisaidia EACC katika uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha za kaunti hiyo. Hatua hii inafuatia uchunguzi ambao EACC imekua ikiendesha kwa muda sasa ikidai huenda kulikuwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni 2 chini ya uongozi wa gavana Obado. Hata hivyo EACC haijatoa taarifa kamili kuhusu lengo la uvamizi huo.

Show More

Related Articles