HabariPilipili FmPilipili FM News

Pwani Hakuna Visa Vya Udanganyifu Wa KCSE Asema Kipsang.

Katibu katika wizara ya Elimu Belio Kipsang ameonyesha kuridhishwa na jinsi mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE  unavyoendelea eneo hili la pwani.

Akizungumza mapema leo wakati wa kukagua zoezi la kusambaza mtihani huo eneo la Kanamai, Majengo kaunti ya Kilifi Kipsang anasema kufikia sasa bado hakujashuhudiwa visa vya wizi wa mtihani eneo hili la pwani ikilinganishwa na sehemu nyingine nchini.

Kufuatia msako wa magari ya uchukuzi wa umma unaoendelea kote nchini Kipsang amepongeza wakuu wa shule kwa kutoa mabasi yao ya shule kusaidia watahiniwa wanaosafiri kutoka sehemu moja hadi nyinbgine.

Show More

Related Articles