HabariPilipili FmPilipili FM News

Hali Ya Usafiri Yabaki Changamoto Mombasa.

Hali ya usafiri wa umma imesalia changamoto kuu kwa wengi katika sehemu mbalimbali za nchi kufuatia msako unaoendelea dhidi ya magari yasiofuata sheria.

Wasafiri wamekuwa na hisia mseto kuhusina na msako huo wamelalamikia kuhangaika kutokana na hali hiyo, Baadhi wakiitaka serikali kutolegeza kamba kuona kuwa nidhamu inadumishwa barabarani.

Kufikia sasa ni matatu moja tu inayohudumu mjini Mombasa katika eneo la Bamburi kuja mjini huku magari mengine bado yakiwa hayajarudi barabarani.

Show More

Related Articles