HabariPilipili FmPilipili FM News

Mtahiniwa Afanyia Mtihani Wa KCSE Hospitali Voi.

Huku mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne ukiingia siku ya 7 leo Mtahiniwa mmoja  kutoka ya shule ya upili ya wasichana ya Voi, ataendelea kufanyia mtihani wake katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi  baada ya kujifungua hospitalini humo hapo jana.

Haya yemethibitishwa na Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Taita Taveta philip Wambua.

Hata hivyo Wambua anasema huenda mtahiniwa huyo akaruhusiwa kuenda nyumbani , huku akizitaka idara husika kuwajibikia swala hilo ili kuhakikisha mshukiwa anachukuliwa hatua za kinidhamu.

 

 

Show More

Related Articles