HabariMilele FmSwahili

Magari ya uchukuzi wa umma yaongezeka barabarani

Msako dhidi ya magari ya uchukuzi wa umma yasiyozingatia sheria za trafiki umeingia siku ya pili leo. Maafisa zaidi wa usalama wanashika doria ili kuwatambua madereva na utingo wasiozingatia sheria hizo. Kinyume na ilivyokuwa jana idadi ya magari ya uchukuzi imeongezeka bara barani leo baada ya wadau katika sekta ya matatu kutangaza kusitisha mgomo wao jana na kukubali kufuata sheria za michuki kufuatia makubaliano baina yao na serikali. Baadhi ya abiria wanaoegemea usafiri wa magari ya umma hapa jijini Nairobi pia wakifurahia kuweza kulipa nauli kama kawaida.

Hawa hapa ni baadhi ya madereva ambao wametii sheria za trafiki maarufu michuki

Wakati huo huo waziri wa usalama dr Fred Matiangi anasema  magari ya uchukuzi wa umma yanayotoza nauli maradufu yatanyanganywa leseni. Matiangi anasema ni sharti Sacco zinazosimamia magari haya kutenga nauli kwa mujibu wa sheria na umbali wa barabara inayotumika.

Show More

Related Articles