HabariMilele FmSwahili

Abiria watatizika, wahudumu wa matatu wakiamua kuondoa magari barabarani

Shughuli za uchukuzi zimetatizika katika maeneo kadhaa hapa jijini Nairobi asubuhi kufuatuia kuanza msako unaolenga kuyaondoa magari na wahudumu wanaokiuka sheria za trafiki maarufu za Michuki. Hii ni baada ya wahudumu wa matatu kuyaondoa bara barani magari yao kulalamikia kutekelezwa sheria hizo.

Baadhi ya wahudumu tuliozungumza nao hata hivyo wameunga mkono haja ya kutekelezwa sheria hizo.

Abiria nao wamelazimika kutembea mwendo mrefu huku wengine wakilazimiki kulipa nauli ya zaidi ya shilingi 200. Wengi wao pia wanalamikia kuchelewa kufika kazini.

Hali sawa imeshuhudiwa mjini Mombasa. Mshirikishi wa kanda ya Pwani Bernard Leparmarai ameshikilia kuwa hakuna mhudumu au gari litakaloruhusiwa bara barani pasi na kufuata sheria.

Show More

Related Articles

Check Also

Close