Swahili Videos

Waziri Matiang’i aonya msako barabarani kuanza kwa kishindo


Mtafaruku wa usafiri wa umma unanukia kuhusiana na msako mkubwa unaotarajiwa kuanza Jumatatu wiki ijayo dhidi ya  magari ya umma na hata yale ya kibinafsi yasiyozingatia kanuni za usafiri.
Hatua hii inajiri baada ya waziri wa usalama wa ndani dakta Fred Matiang’i na waziri wa uchukuzi James Macharia kutoa onyo kuwa msako huo utakuwa wa kufa kupona.
Kwa upande wao wahudumu wa uchukuzi wa umma wanasema huenda wakasusia biashara kwa muda ili kutathmini hali itakavyokuwa.

Show More

Related Articles