HabariPilipili FmPilipili FM News

Mdudu Achora 666 Ndani Ya Nyumba Kikambala Kaunti Ya Kilifi.

Wananchi katika eneo la Kikambala kaunti ya Kilifi wameachwa na mshangao baada ya kupata mdudu kwa jina vunja-jungu almaarufu prayingmantis akiwa amechorwa alama ya 66 mara 6 katika nyumba ya mwanajamii mmoja.

Edwin Mwendo ambaye amekumbana na mdudu huyo ameeleza kushangazwa na tukio hilo  na kuwaarifu majirani hasa baada ya kuona kuwa ana alama hizo za waabudu shetani.

Nambari hizo zilikuwa zimeandikwa kwa rangi Nyeusi,nyeupe na kijani kibichi.

Mwendo hata hivyo amewaarifu viongozi wa kidini  ambao walikuja katika eneo hilo na kufanya maombi.

Show More

Related Articles