HabariPilipili FmPilipili FM News

Afueni Kwa Wananchi Kwani Sasa Wataweza Kuwaripoti Maafisa Wapolisi Wanaovunja Sheria.

Idara ya polisi imezindua mfumo maalum ambapo wananchi sasa wanaweza kutoa ripoti kuhusu maafisa wa polisi wanaovunja sheria.

Mfumo huo ambao uko chini ya wizara ya masuala ya ndani unajulikana kama Anonymous Reporting Information System.

Chini ya mfumo huo wanachi wataweza kutuma ujumbe mfupi bila malipo kwa nambari 40683, au kupiga simu bila malipo kwa nambari 0800721230, ambapo walalamishi watapewa nambari ya siri ya ufuatilizi wa lalama zao.

Watetezi wa haki za binadam wamekuwa wakishinikiza mfumo huo kuzinduliwa, ili kusaidia katika uchunguzi pale kunapotokea uhalifu miongoni mwa maafisa wa polisi au hata jamii

Show More

Related Articles