HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughli Za Uvuvi Katika Kanda Ya Pwani Zarejelea Kawaida

Shughuli za uvuvi Pwani Kaskazini zimeanza kuimarika hii ikiwa ni baada ya bahari hindi kurejea hali yake ya kawaida.

Gambo Kanyoe ambaye ni miongoni mwa washikadau wa uvuvi anasema tayari wavuvi kutoka Pemba na Shimoni ,wameanza kushuhudiwa katika maeneo ya Mayumgu, Wesa na hata bandari ya Old Ferry mjini Kilifi na wanaendelea kuvua samaki katika maji makuu.

Shallo Issa ambaye ni miongoni mwa wavuvi kaunti ya kilifi anasema sasa kiwango cha samaki kinachovuliwa  kimefikia tani tatu kwa siku, na kwamba huenda kiwango hicho kikaongezeka  .

Anasema aina za samaki wanaopatikana kwa wingi ni Tuna,Tafi,jodari, pweza miongoni mwa aina nyengine ya samaki.

Show More

Related Articles