HabariMilele FmSwahili

Raila :Kenya ina uhaba mkubwa wa nyumba za makaazi

Kenya ina uhaba mkubwa wa nyumba za makaazi. Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu miundo Msingi, Raila Odinga hata hivyo anasema mradi wa serikali wa ujenzi wa makaazi kwa bei nafuu utawanufaisha wakenya pakubwa iwapo utatakelezwa kikamilifu. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa makaazi huko Thindigwa, kaunti ya Kiambu, Raila anasema kila mkenya ana haki ya kupata makaazi hayo.

Raila ametaka ushirikiano wa karibu baina ya serikali kuu, zile za kaunti na washirika wa kibinfasi kumwezesha rais Uhuru Kenyatta kutekeleza mradi huo.

Mradi huo wa nyumba utagharimu takriban shilingi bilioni 2.1.

Show More

Related Articles