HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanafunzi Wajipata Katika Hali Ya Sinto Fahamu Baada Ya Kugundua Hawa kusajiliwa Katika Somo Moja.

Kufikia sasa eneo la taita-taveta hakujashuhudiwa kisa chochote cha udanganyifu katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne inayoendelea.

Haya yamebainishwa na afisa wa elimu katika gatuzi la Taveta Abdulrahman Hassan na kuongeza kuwa watahiniwa watatu   wamekosa kukalia mtihani mmoja baada ya kusajili somo ambalo hawakusomea kimakosa.

Abdulrahman aidha amesema katika eneo hilo hakujakuwa na watahiniwa kufanyia mtihani katika hospitali, baada ya kujifungua ila amedhibitisha kuweko na visa viatatu vya mimba katika shule ya Eldoro,Lumi na Bishop Njenga.

Hata hivyo amesema idara yake ikishirikiana na washikadau waelimu itafanya mkao wa kuhamasisha jamii  kuhusiana na adhari za mimba za mapema kwa wanafunzi.

Show More

Related Articles