HabariMilele FmSwahili

Polisi kuanza kupokea marupurupu ya nyumba kuanzia mwezi ujao

Polisi wataanza kupokea marupurupu ya nyumba kuanzia mwezi ujao. Hatua hii ikilenga kuhakikisha maafisa wa usalama wanatangamana na umma.Waziri wa usalama  wa ndani dr Fred Matiangi aliyetangaza mpango huo anasema idara ya polisi inajitahidi kutekeleza kikamilifu mabadiliko yaliyotangazwa na rais Uhuru Kenyatta katika idara hiyo.

Matiangi pia amezindua kitengo maalum kitachopokea malalamishi kutoka kwa umma kuhusu utendakazi wa maafisa wa polisi.

Amevitaka vitengo mbali mbali vya usalama kuwajibikia majukumu yao kwa kuzingatia maadili na nidhamu.

Show More

Related Articles