HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Wa Kidini Wataka Wanaowatunga Watoto Mimba Kuchukuliwa Hatua Kali.

Viongozi wa kidini ni wa hivi punde kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria watakaopatikana kuchangia mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi waliofanya mtihani wao wakiwa wajawazito na hata wengine kujifungua wwakati wa mtihani.

Akizungumza kwenye kongamano la Kamati kuu ya ya makanisa ya Kianglikana mjini Malindi, Askofu Lawrence Dena wa kanisa hilo ,ameilaumu jamii akisema imefeli katika kuwakuza watoto kwenye maadili mema , hali ambayo anadai ndio chanzo cha idadi kubwa ya mimba za mapema kushuhudiwa.

Show More

Related Articles