HabariMilele FmSwahili

Watahiniwa 19 katika shule ya upili ya Oloolasir Kajiado wakamatwa kwa kuzua vurugu shuleni

Watahiniwa 19 katika shule ya upili ya Oloolaisir kaunti ya Kajiado wamekamatwa baada ya kuzua vurugu usiku wa kuamkia leo na kusababisha uharibufu wa mali shuleni humo. Watahiniwa hao wanatarajiwa mahakamani leo huku mikakati ikiwekwa kuwawezesha kuendelea na mtihani wao. Chanzo cha vurugu za wanafunzi hao hakijabainika. Hata hivyo inaarifiwa huenda zilichangiwa na kutoweza kwao kushiriki udanganyifu.

Show More

Related Articles