HabariPilipili FmPilipili FM News

Kipindu pindu Chakodolea Macho Wakaazi Wa Kongowea Kutokana Na Mirundiko Ya Taka.

Wakazi wa Karama Kongowea kaunti ya Mombasa wanaishi kwa hofu ya kupatwa na maradhi hatari kama vile kipindu pindu kutokana na jaa la taka lililoko eneo hilo.

Baadhi ya wanabiashara tulioweza kuzungumza nao, wanasema wameathirika pakubwa na jaa hilo, ikiwemo ambalo kupungua kwa wateja wao kufuatia uwepo wa mazingira chafu pamoja na harufu mbaya.Kulingana nao wakati mwingine vijusi pia vimekuwa vikitupwa eneo hilo.

Wakazi eneo la karama sasa wanaitaka serikali kuu na ile ya kaunti kushugulikia swala hilo kwa haraka ili kuwaondolea dhiki ya uvundo mkali pamoja na hatari ya kuambukizwa maradhi yatokanayo na uchafu.

Show More

Related Articles