HabariPilipili FmPilipili FM News

Zaidi Ya Makurutu 3,000 Wa KDF Wafuzu Hii Leo.

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wanajeshi wa KDF kuzidi kudumisha nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuilinda taifa.

Akiongea wakati wa kufuzu kwa makurutu wa jeshi la KDF mjini Eldoret, rais Kenyatta amesistiza usalama wa kenya unapaswa kupewa kipaombele na kila mmoja wao kuhakikisha wakenya wako salama kila wakati.

Wakati huo huo rais amesema wanajeshi hao wanajiunga na kikosi hicho wakati ambapo taifa linawahitaji zaidi ambapo wanahitajika kuisoma vyema na kuilinda mipaka ya taifa hili.

 

Show More

Related Articles