HabariPilipili FmPilipili FM News

Maambukizi Ya Maradhi Ya Zinaa Yaongezeka Miongoni Mwa Vijana.

Maambukizi ya maradhi ya zinaa pamoja na yale ya  ukimwi yanaendelea  kuongezeka hususan kwa vijana wa kati ya umri wa miaka 14 hadi 18.

Afisaa mkuu wa afya ya jamii kaunti ya mombasa Aisha Abbakar anasema asilimia kubwa ya vijana, wamekuwa  wakikataa kwenda hospitali kupata matibabu ya maradhi hayo na pia kupima , kutokana na wao kuhofia kujulikana na  kutegwa katika jamii.

Akiongea kwenye hafla ya kuwahamasisha vijana juu ya mimba za mapema na  afya yao kwa ujumla hapa mombasa,  Aisha anasema kaunti hii imeweka mikakati mpya kuhamasisha vijana kupitia vijana wenzao, ikiwemo kuweka  vituo maalum vya matibabu ya maradhi yatokanayo na kujamiana  ili kusaidia vijana

Show More

Related Articles