HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Kaatika Kaunti Ya Lamu Wapongeza Mradi Wa Kuweka Mataa Ya Barabarani.

Hatua ya Shirika la Kenya Power kutia saini mkataba na Serikali ya Kaunti ya Lamu kuweka mataa ya barabarani unaendelea kupongezwa na washikadau mbalimbali wa Kaunti hiyo.

Waziri wa Kawi Fahima Araphat Abdalla amekuwa wa hivi punde kusema mataa hayo yatawezesha utekelezwaji wa miradi mbalimbali inayoendelezwa eneo hilo, ukiwamo wa Lappset, na ule wa makaa ya mawe.

Araphat anasema mradi huo pia utasaidia kuthibiti visa vya uhalifu, hasa katika maeneo ya Witu, Mpeketoni na Mokowe.

Show More

Related Articles