HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wa Wizi Wa Mitihani Kufikishwa Mahakamani Leo.

Washukiwa wawili wakuu wa wizi wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE unaoendelea nchini watafikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya jaribio la wizi wa mtihani huo.

Waziri wa elimu Amina Mohamed anasema wawili hao walikamatwa hapo jana, katika oparesheni iliyoendeshwa na polisi kwa ushirikiano na maafisa wa baraza la mitihani nchini KNEC.

Amina anasema wawili hao wanaaminika kuwa miongoni mwa walanguzi wakuu wa mitihani ya kitaifa, ambao wamekuwa wakitekeleza uhalifu huo kwa mda wa miaka miwili  iliyopita.

Show More

Related Articles