HabariMilele FmSwahili

Polisi 3 wa akiba wauwawa na majangili eneo la Kalau Meru

Polisi watatu wa akiba wameuwawa baada ya kuvamiwa na majangili katika eneo la Kalau huko  Igembe ya kati kaunti ya Meru. Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia kisa hicho. Wakati uo huo mtu mmoja amepoteza uhai na wawili wamejeruhiwa vibaya kufuatia mapigano baina ya watu wa koo mbili huko Qara kaunti ya Wajir. Kamanda wa polisi Wajir Stephen Ngetich amedhibitisha kuwa mapigano hayo yamechochewa na uhasama kuhusiana na maeneo ya kulisha mifugo.

Show More

Related Articles