HabariPilipili FmPilipili FM News

Ushirikiano Wa Kenya Power Na Kaunti Ya Lamu Wapongezwa.

Hatua ya Shirika la Kenya Power kutia saini mkataba wa makubaliano na Serikali ya Kaunti ya Lamu ya utekelezwaji wa mradi wa kuweka mataa ya mtaani kwenye maeneo mbalimbali ya mji huo unaendelea kupongezwa na washikadau mbalimbali wa Kaunti hiyo.

Waziri wa Kawi Fahima Araphat Abdalla amekuwa wa hivi punde kusema kuwa mataa hayo yatawezesha utekelezwaji wa miradi mbalimbali inayoendelezwa eneo hilo ukiwamo wa Lappset, Coal Plant miongoni mwa mingine kufanyika kwa njia ya urahisi zaidi.

Kadhalika ameeleza Imani ya visa vya utovu wa usalama mabvyo vimekuwa vikishuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo ya Kaunti hiyo kupungua kwa asilimia kubwa.

Siku sita zilizopita Shirika la Kenya Power na Serikali ya Kaunti hiyo zilitia saini mkataba wa mradi huo utakaoigarimu Serikali ya Kitaifa shilingi milioni 53 unaonuiwa kunza kutekelezwa hivi karibuni kwenye maeneo ya Witu, Mpeketoni na Mokowe.

 

Show More

Related Articles