HabariMilele FmSwahili

Washukiwa wakuu wa udanganyifu katika mtihani wa KCSE kufikishwa mahakamani asubuhi hii

Watu 19 wamekamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na jaribio la udanganyifu katika mtihani wa KCSE unaoingia siku ya nne leo. Waziri wa elimu Balozi Amina Mohamed anasema watu 15 walikamatwa katika kaunti ya Kisii huku wanne wakinaswa huku Kakamega. Amina washukiwa wakuu wawili wa njama hiyo nchini watafikishwa mahakamani asubuhi hii. Akizungumza alipoongoza ufunguzi wa makasha ya karatasi za mtihani huo katika mtaa wa Langatta hapa Nairobi waziri Amina hata hivyo ameshikiliwa kuwa hakuna kisa chochote cha wizi wa mtihani kilichoripotiwa kufikia sasa.

Kadhalika amewaonya walimu dhidi ya kuhusika katika jaribio lolote la kuhujumu uadilifu wa mtihani huo huku pia akitangaza masharti mapya ya kudhibiti udanganyifu.

Show More

Related Articles