HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Viwanja Vya Ndege Hapa Nchini Watajwa Kuwadhalilisha Watalii.

Wahudumu wa viwanja vya ndege humu nchini wanaowaelekeza na kukaribsisha wageni wanaozuru taifa hili wametakiwa kuzingatia maadili na kuwaelekeza wageni kwa njia inayofaa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Moi hapa mombasa waziri wa utalii Najib Balala amesema baadhi ya wahudumu katika viwanja vya ndege huwadhalilisha watalii badala ya kuwahudumia ipasavyo.
Balala ametoa wito kwa mamlaka ya ndege nchini kutatua suala hilo kuona kuwa sekta ya utalii inaimarika hata zaidi.

Show More

Related Articles