HabariMilele FmSwahili

Uchunguzi waanzishwa kubaini chanzo cha mkasa wa moto katika Soko la Gikomba

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha mkasa wa moto ulioteketeza zaidi ya vibanda 6 katika soko la Gikomba mwendo wa saa 9 alfajiri ya leo. Akizungumza baada ya kuzuru eneo la mkasa naibu kaunti kamishna wa Nairobi Moses Lilan amedhibitisha kuwa hakuna aliyejeruhiwa. Pia amesema moto huo umedhibitiwa.

Kadhalika Lilan amewataka wafanyibiashara hao ambao wanadai kulipwa fidia kusubiri hadi uchunguzi ukamilike.

Show More

Related Articles