HabariPilipili FmPilipili FM News

Wapangaji Wagura Kisauni kwa Kuhofia Usalama Wao.

Kufuatia kukithiri kwa makundi ya uhalifu katika eneobunge la kisauni, wamiliki wa nyumba za kukodisha eneo hilo sasa wanakadiria hasara kwa kukosa wapangaji.

Yusuf Hajj ambaye ni mwathiriwa kutoka Mtaa wa Town Down Bakarani anaeleza kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja nyumba zake zimesalia mahame kutokana na wapangaji kuhofia usalama wao katika mtaa huo.

Yakijiri hayo familia moja inaendelea kuomboleza kifo   cha mpendwa wao aliyevamiwa na kushambuliwa na wahuni usiku wa kuamkia jumatatu.

Samson Kinuthia Karanja mwenye  umri wa miaka 42 na baba wa watoto watatu alivamiwa na wanachama hao waliomkata mara kadha kwa panga kichwani

Show More

Related Articles