HabariPilipili FmPilipili FM News

Kanisa Katoliki Laendelea Kuomboleza Kifo Cha Askofu Njenga.

Viongozi mbalimbali wa kanisa katoliki hapa Mombasa wanaendelea kuomboleza kifo cha askofu Johna Njenga aliyefariki siku ya Jumapili katika hospitali ya Mater huko Nairobi.

Padri Wilbard Lagho pamoja na waumini wa kanisa katoliki wamemsifia Askofu Njenga, hasa kutokana na mchango wake mkuu kwa sekta ya elimu ya dini.

Padri Lagho Amesema ilikua kama jukumu la Marehemu kuwapeleka mapadri shuleni kuendeleza masomo yao.

Father  Wilbard ameongeza kuwa  askofu Njenga alikuwa mtu mcheshi,mkarimu na mwenye utu.

Alikuwa ni kiongozi mwenye busara na alifanya kazi pamoja na wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia katika jamii.

Show More

Related Articles