Pilipili FmPilipili FM News

15 Wakamatwa Kwa Jaribio La Wizi Wa Mtihani Wa KCSE.

Kufikia sasa wasimamizi 15 wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne wamekamatwa na polisi kwa jaribio la wizi wa mtihani huo ulioanza rasmi hapo jana.

Kulingana na baraza la mitihani nchini KNEC ,wote hao walikamatwa maeneo ya Nyanza na Magharibi mwa nchi  wakijaribu kupenyeza karatasi za mtihani wa KCSE katika shule mbili za  maeneo hayo.

Mapema hapo jana mwenyekiti wa baraza la mitihani nchini George Magogha alitoa hakikisho kwamba mtihani huo utafanyika kwa uadilifu bila visa vya wizi kushuhudiwa.

Show More

Related Articles