HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Mombasa Waombwa Kuchukua Mikopo Ili Kujiendeleza Kiuchumi.

Kaunti ya mombasa imeorodheshwa miongoni mwa sehemu zenye idadi ndogo ya watu wanaochukua mikopo kutoka kwa serikali, kupitia mfuko wa pesa za vijana almaarufu Youth Fund, mfuko wa pesa ya kinamama pamoja na revolving Fund inayotolewa chini ya serikali za kaunti.

Francis Thoya ambaye ni katibu wa serikali ya kaunti ya mombasa anasema hali hiyo imetokana na wananchi kuogopa madeni.

Thoya ametoa changamoto kwa jamii hususan vijana na kinamama kuchukua mikopo hiyo kujiajiri hatua ambayo anasema itasaidia kukuza uchumi.

Hata hivyo amesema wanaochukua miokopo hiyo watafanyiwa ukaguzi wa kina baada ya kubainika kuwa wengi kati ya wanaochukua mikopo hiyo hawalipi madeni yao kama inavyo stahili.

Show More

Related Articles