HabariMilele FmSwahili

Mshukiwa wa 3 kwenye mauaji ya Monica Kimani Jennings Orlando aachiliwa huru

Mshukiwa wa 3 kwenye mauaji ya Monica Kimani Jennings Orlando ameachiliwa huru.Jennings ambaye alikamatwa  mwezi jana amewekwa huru baada ya  kukamilika kwa siku 14  walizopewa polisi kukamilisha uchunguzi dhidi yake.Hatua hiyo pia imechangiwa na afisa aliyekuwa akiendesha  uchunguzi dhidi yake Maxwel Otieno  kuondoa ombi la kutaka aendelee kuzuiliwa.Jennings ambaye alifikishwa  mbele ya hakimu Stella Atambo ameagizwa kuripoti katika afisi za DCI kila jumatano kwa muda wa miezi 2.Orlando anadaiwa kuwa na mshukiwa mkuu wa mauaji  ya Monica Joseph Irungu wakati wa mauaji hayo na sasa atatumika kama shahidi.

Show More

Related Articles